DSpace Repository

Uhakiki wa fani ya muundo na matumizi ya lugha ya Diwani za kishairi za Said Ahmed Mohamed

Show simple item record

dc.contributor.author Nyabuya, Richard Atuti
dc.date.issued 2014-10
dc.date.accessioned 2019-03-05T12:26:50Z
dc.date.available 2019-03-05T12:26:50Z
dc.identifier.uri http://41.89.96.81:8080/xmlui/handle/123456789/1502
dc.description.abstract Utafiti huu ulinuia kuhakiki fani katika diwani za ‘Sikate Tamaa, Kina cha Maisha na Jicho la Ndani za Said Ahmed Mohamed kwa kutumia mkabala mpya wa kuchunguza ushairi wa Kiswahili. Mkabala huu unazingatia uhalisi wa ushairi wa Kiswahili kuwa una tagaa mbili kuu ambazo ni ushairi funge na ushairi huru, wala si ushairi funge tu kama ambavyo imezoeleka kwenye chunguzi nyingi. Diwani hizi, kwa kusheheni mashairi huru na funge badilifu ya mtunzi mmoja, ni za kipekee katika ushairi wa Kiswahili. Fani tuliyoichunguza ni ya muundo na matumizi ya lugha kama inavyodhihirika katika mashairi huru na funge ya mtunzi wa diwani hii. Uchanganuzi wa kithamano ulitumika katika utafiti huu. Madhumuni ya utafiti huu ni kutambua na kuelezea muundo wa mashairi ya Said Ahmed Mohamed yaliyomo katika diwani hizi nakubainisha mbinu za lugha alizozitumia katika kuyasuka mashairi yake ili kuonyesha namna hili huchangia kuleta maana ya shairi. Pia, utafiti huu ulinuia kuonyesha iwapo fani ya mtunzi tunayoishughulikia inaonyesha kukua. Nadharia ya Umuundo iliongoza utafiti huu. Nadharia hii ilituwezesha kudondoa na kuelezea vipengele vya fani ya muundo vijengavyo mashairi yaliyoshughulikiwa. Pia, nadharia hii ilitusaidia kubainisha vipengele vya lugha ambavyo vinashirikiana kuunda mashairi ili yalete maana. Hili limechangia uelewekaji wa muunganiko wa ndani wa mashairi yaliyochunguzwa na maendeleo ya mtunzi katika fani. Mbinu ya uteuzi wa kimakusudi ilitumika katika kukusanya sampuli ya mashairi kwa minajili ya uchunguzi. Ukwasi mkubwa wa fani ya muundo na matumizi ya lugha kwenye diwani zetu za utafiti umedhihiri katika uchunguzi huu. Utafiti huu, tena, umeonyesha kuwa ushairi wa Kiswahili unaweza kueleweka na kuthaminika iwapo fani yake itachambuliwa kwa undani. Pia, utafiti huu umebainisha kuwa sanaa ni kitu hai na uhai huu umedhihirishwa katika fani ya muundo na matumizi ya lugha ya diwani za kishairi za Said Ahmed Mohamed ambapo fani hii imeonyesha kukua. Mwisho, ubainisho wa mbinu mbalimbali za utunzi wa mashairi katika utafiti huu, tunatumai, utawafaa watunzi na wasomi wengi wa ushairi wa Kiswahili. *** This research aimed at critically analyzing form in ‘Sikate Tamaa, Kina cha Maisha and Jicho la Ndani anthologies of Said Ahmed Mohamed by use of a new approach to studying Swahili poetry. This approach takes into consideration the reality of Swahili poetry as having two main branches which are prosodic and free verses and not only prosodic as is commonly reflected in many studies. These anthologies, by comprising both prosodic and free verses of variety of forms composed by same author, are unique in Swahili poetry. Structure and language use are the form elements that were examined as are manifested in both free and prosodic verses of the author of this anthologies. Qualitative analysis was employed in this research. The objectives of this research were to identify and explicate the structure of the poems of Said Ahmed Mohamed in these anthologiesandclarify the aspects of language use to show how this contributes to bringing out meaning of a poem. The research also intended to show progress of the authors form. The theory of Structuralism guided this research. This theory enabled us pick structural form elements involved in construction of the poems and elucidate them. The theory also assisted us clarify language aspects that are collectively involved in the composition of the poems to bring out meaning. This analysis contributes to the understanding of the internal linkages of the poems under investigation and shows growth in the authors form. Purposive sampling technique was employed in the collection of poems for analysis. Immense richness in structure and language use in our research anthologies has been made manifest. The research, also, reveals that Swahili poetry can be understood and valued with deep analysis of its form. Again, the research shows growth and development nature of art in structure and language use in the poetic anthologies of Said Ahmed Mohamed. Finally, we hope the revelation of different ways of verse composition in this research will be of great benefit to many Swahili poetry composers and scholars. en_US
dc.language.iso en en_US
dc.publisher Egerton University en_US
dc.subject Lugha -- Diwani za kishairi en_US
dc.title Uhakiki wa fani ya muundo na matumizi ya lugha ya Diwani za kishairi za Said Ahmed Mohamed en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Browse

My Account