DSpace Repository

Utambulisho wa mwanamume katika methali za jamii ya Agikuyu

Show simple item record

dc.contributor.author Gichohi, Francis Gichini
dc.date.issued 2018-04
dc.date.accessioned 2019-03-05T12:35:14Z
dc.date.available 2019-03-05T12:35:14Z
dc.identifier.uri http://41.89.96.81:8080/xmlui/handle/123456789/1503
dc.description.abstract Utafiti huu ulichunguza Utambulisho wa mwanamume katika methali za Agikuyu. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kudhihirisha jinsi jamii ya Agikuyu walivyomtambulisha mwanamume kupitia methali. Pia utafiti huu ulidhamiria kubainisha majukumu na nafasi ya mwanamume kama inavyodhihirika katika methali hizo. Msingi wa kinadharia alioutegemea mtafiti ulikuwa Nadharia ya Uchanganuzi Hakiki Usemi Mkabala wa Kihistoria. Nadharia hii inahusika na uchanganuzi wa miundo ya lugha inayodhihirisha ubaguzi. Nadharia hii ina mikakati mitano ambayo ndiyo iliyotumika kama mwongozo wa uchanganuzi wa data. Mkakati hiyo ni Urejelezi, Nomino, Ubishi, Mkabala na Kufifiza. Mbinu za utafiti huu zilikuwa utafiti wa kimaktaba na utafiti wa nyanjani. Data ya utafiti huu ilipatikana kutoka kwa methali teule arobaini na tano za jamii ya Agikuyu zilizochanganuliwa. Katika kuichanganua data mtafiti alitumia maelezo na majedwali kufafanua matokeo yaliyopatikana. Matokeo ya utafiti huu yalidhihirisha kukwezwa kwa mwanamume na kutambuliwa kwa njia ya kipekee na kutwezwa na kudhalalishwa kwa mwanamke. Kila mkakati ulichunguzwa kibinafsi na kudhibitisha kuwa matumizi ya lugha yalidhihirisha ubaguzi. Utafiti ulidhibitisha kuwa mwanamume amepewa majukumu yanayomsawiri kwa njia chanya na kuonekana kuwa nguli, ilhali mwanamke amefifizwa. Utafiti huu ni muhimu kwa watafiti wa lugha hasa katika uwanja wa isimu, ikizingatiwa kuwa ni utafiti wa kiisimu. Pia ni mchango muhimu katika uhifadhi wa Fasihi Simulizi ya Wakikuyu katika maandshi. Taasisi ya maswala ya kijinsia pia yatanufaishwa na utafiti huu. Mwisho utafiti huu ni mchango mpya katika tafiti za baadaye za uchanganuzi wa lugha na kuendeleza uwanja mpana wa isimu. Mtafiti amependekeza kuwa kuwe na usawa wa kimenke katika kugawanya majukumu na nafasi katika jamii. Pia mtafiti anapendekeza mahusiano ya uana yawe mazuri na yenye usawa. Nao watetezi wa usawa wa kijinsia wawajibike katika kuleta usawa wa kijinsia miongoni mwa wanajamii. This research was on analysis of identity of man in Kikuyu proverbs. The aim of this research was to examine in details how language is used to identify a man in kikuyu proverbs. The theoretical framework of this research was Historical Discourse Approach. This theory has five discursive strategies that guided the researcher in data analysis. The strategies include Referential, Predicational, Argumentation, Perspectivation and Mitigation. Referential strategy looked at how persons are named and referred to linguistically. Predicational strategy looked at the traits, characteristics, qualities and features attributed to them. Argumentation strategy looked at argumentation schemes, that is, how persons try to justify and legitimize the exclusion and discrimination of others. Perspectivation strategy looked at point of view of these strategies. Finally the mitigation strategy focused on whether the utterance were articulated overtly or covertly. The main basis of this theory are positive self and negative other presentation. The research design and method of data collection was textual analysis. The data for this research was forty five (45) selected proverbs of the Agikuyu community. They were analysed on how they identified a man in the Agikuyu community and how they depicted gender roles. The identity and the gender roles were analysed on the basis of political, economical, social, physical and psychological aspects. The results were presented descriptively and in tabular form. The results ascertained that proverbs of Agikuyu community identifies a man as a superior being compared to a woman. The gender roles based on political, economical, social, physical and psychological aspects were also identified. The roles indicated that the male gender had more superior roles, hence, portraying him to be of a higher status than the female. The findings of this research are expected to be a major contribution in the preservation of the Kikuyu oral literature through documentation.The findings will also be of a great contribution to gender studies. They will be a new contribution in the field of discourse analysis and moreover they will form a basis for further research in this area. The researcher recommends for further research on the Agikuyu community and more documentations of their oral literature. en_US
dc.language.iso en en_US
dc.publisher Egerton University en_US
dc.subject Methali -- Jamii ya Agikuyu en_US
dc.title Utambulisho wa mwanamume katika methali za jamii ya Agikuyu en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Browse

My Account