DSpace Repository

Uwakilishaji wa utandawazi katika riwaya mpya ya kiswahili iliyoandikwa na Said A. Mohamed na Wadi K. Wamitila

Show simple item record

dc.contributor.author Alomo, Seth Ochieng’
dc.date.issued 2016-08
dc.date.accessioned 2019-03-05T12:41:20Z
dc.date.available 2019-03-05T12:41:20Z
dc.identifier.uri http://41.89.96.81:8080/xmlui/handle/123456789/1504
dc.description.abstract Utandawazi ni suala ambalo kwa kipindi kirefu lilisawiriwa na waandishi wa riwaya kama wakala wa maendeleo. Maendeleo haya yalifasiriwa kama utangamano wa watu kimataifa kwa misingi ya kijamii, kiuchumi na kisiasa. Hata hivyo, uwakilishi wake katika Riwaya Mpya ya Kiswahili umechukua mkondo mpya. Hii ni kwa sababu ya waandishi kuuangaza kwa kutumia vipengele vya Usasaleo na Udenguzi. Nia ya kutumia vipengele hivi katika Rawaya Mpya si wazi. Aidha, sababu ya kuvitumia kuwakilisha utandawazi si bayana. Utafiti huu ulihakiki matumizi ya elementi za Usasaleo katika kujenga maudhui ya utandawazi na nia ya matumizi yao. Nadharia ya Usasaleo iliongoza utafiti huu kwa sababu ya mihimili yake. Nadharia ya Usasaleo inapinga na kuyaumbua masuala mengi yaliyozingatiwa katika enzi ya Usasa. Inampa mtumizi wake uhuru wa kujaribu mbinu mpya bila ya kubanika katika sheria za sanaa zilizozingatiwa katika enzi za Usasa. Uteuzi wa sampuli ulikuwa wa kimaksudi ili kushughulikia uwakilishi wa waandishi kuhusuutandawazi. Riwaya hizi zilijumuisha: Bina- Adamu (Wamitila, 2002) Musaleo! (Wamitila, 2004) Dunia Yao (Mohamed, 2006) na Babu Alipofufuka (Mohamed, 2001). Mbinu ya uchanganuzi ilihusu yaliyomo katika Riwaya Mpya ya Kiswahili. Uchanganuo wa yaliyomo ulimwezesha mtafiti kuchanganua maudhui yaliyoingiliana na utandawazi ili kuonyesha uwakilishi wake. Utafiti huu ulibainisha kuwa; suala la utandawazi limewasilishwa kupitia maudhui mbalimbali ya Riwaya Mpya. Uwasilisho huu ulikuwa wa moja kwa moja au usio wa moja kwa moja. Vilevile, maudhui haya yaliwasilishwa kwa kutumia vipengele vya Usasaleo. Vipengele hivi vilijumuisha; uhalisia-ajabu, uasi, na mwingiliano matini, Aidha, mitazamo ya waandishi kuhusu suala la utandawazi ilidhihirishwa kupitia matumizi ya lugha yakiwemo tamathali mbalimbali za fasihi.Utafiti huu utafaidi wanafunzi, walimu, wataalam wa fasihi na Taasisi ya kuendeleza mitaala ya Kenya. ***** Globalisation is a phenomenon that for a long time, different literary writers have portrayed as an agent of rapid development. These developments are perceived to be eminent in the economic, political and social arena of people. Kiswahili novel writers have portrayed the concept of globalisation as integration of people, ideas, culture and values. However, some of Kiswahili novels have taken a new twist in expressing the same concept by using Postmodern elements. These elements which includes; black humor, magical realism, pastiche among others, have complicated the understanding of globalisation making it unclear. Furthermore, the intention of using these techniques in regard to globalisation has added more confusion than clarification. This study therefore, reviewed critically how postmodern techniques had developed themes in relation to globalisation and the intension of the writers towards the same. This research used Postmodernism theory: it deconstructs and refutes many aspects and guidelines that were upheld during the modernist era. This is achieved through the themes and techniques like irony, metafiction, magic realism, intertextuality among others, as used in the novels studied. The methodology involved library study and the sampling procedure was purposive. The novels studied included: Bina- Adamu! (Wamitila, 2002) Musaleo! (Wamitila, 2004) Dunia Yao (Mohamed, 2006) and Babu Alipofufuka (Mohamed, 2001). The internet was also of great significance in data collection for this study. Data analysis was done using content analysis method. The researcher used literary criticism and analysis to study these novels. It was evident in this research that globalisation was presented in different themes of new Kiswahili novel, directly or indirectly. These themes were built in different elements of postmordenism which included magical realism, fabulation, matafiction, intertextuality among others. Furthermore, their intentions about globalisation were evidenced strongly in their figurative language and the techniques of expression used. This research will be beneficial to students, teachers, researchers and the Kenya Institute of Curriculum Development. en_US
dc.language.iso en en_US
dc.publisher Egerton University en_US
dc.subject Utandawazi -- Riwaya en_US
dc.title Uwakilishaji wa utandawazi katika riwaya mpya ya kiswahili iliyoandikwa na Said A. Mohamed na Wadi K. Wamitila en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Browse

My Account