Abstract:
Fasihi ya watoto imepewa urnuhimu mkubwa na wahakiki, wanasaikolojia, wanaelimu-jamii
na wanahistoria. Wametarnbua kwamba ni fasihi iliyo na utajiri, upevu na burudani. Hata
hivyo, fantasia kama mbinu muhimu katika hadithi za watoto haijashughulikiwa kwa dhati na
wahakiki na wasomi. Utafiti huu ulitathmini vipengee vya kifasihi vinavyozua fantasia katika
hadithi fupi za watoto za Nyambura Mpesha. Mbinu ya uchambuzi Wa yaliyomo ikiongozwa
na nadharia ya fantasia ya Bormann (1990) mtumika. Nadharia hii inashikilia kuwa maana ya
ishara zinazotumika katika fantasia husababisha ushirikiano na utangamano. Makisio manne
ya nadharia hii yalitumiwa kuchanganua muundo wa fantasia. Katika utafiti huu, makisio
hayo yalitumika kama mihimili iliyouongoza utafiti katika kuchanganua muundo na
umuhimu wa fantasia katika kazi teule za Nyambura Mpesha (1997 - 2005). Kuafikia haya,
vitabu vinne vya hadithi vilivyoandikwa na mwandishi katika lugha ya Kiswahili vilisomwa
na kuhakikiwa. Deta ya kimsingi iliangazia jinsi vipengee vya kifasihi vinavyotumiwa na
waandishi katika kuibua fantasia katika hadithi za watoto. Palitumika mbinu ya kithamano
katika uchanganuzi wa data na katika kueleza matokeo. Utafiti huu ulitoa mwanga kuhusu
vijenzi vya fantasia na ufaafu wake katika hadithi za watoto. Matokeo ya utafiti huu ni
muhimu madhali utawaelekeza waandishi chipukizi katika kutumia fantasia ifaavyo katika
uandishi wa vitabu bora vya watoto vyenye kuburudisha na kuclimisha.