Abstract:
Wasomaji hupenda kusoma riwaya zilizo na mandhari sahiliz mandhari ya
uhalisia. Hata hivyo watunzi huweza kuandika riwaya zinazotumia mandhari ya
kidhahahania. Wasomaji wa riwaya wanaposoma riwaya inayotumia mandhari ya
kinjozi, wao hutatizika kuelewa kazi hiyo. Tatizo la kimtindo hujitokeza. Utafiti huu
ulichunguza mandhari ya kinjozi yanavyotumiwa kumulika matatizo ya jamii katika
riwaya za Kusadikika na Walenisi. Malengo yalikuwa kubainisha sifa bainifu (za
upekee) za mbinu ya mandhari ya kinjozi katika Kusadikika na Walenisi, kufafanua
namna watunzi wa riwaya za Kusadikika na Walenisi wanavyotumia mbinu hii kumulika
matatizo ya jamii na pia kubainisha utata wa matumizi ya‘ istiara unaosababishwa na
matumizi ya mbinu hii. Nadharia za Uhakiki wa Kimtindo na Uumbuaji ndizo
zilizotumika katika utafiti huu. Deta ilipatikana kwa kusoma na kuchanganua riwaya za
Kusadikika na Walenisi. Pia ingine ilipatikana kwa kuwahoji walimu na wanafunzi wa
shule za upili wilayani Bondo. Deta yenyewe ilikuwa sifa bainifu za mbinu ya mandhari
ya kinjozi katika riwaya za Kusadikika na Walenisi. Deta pia ilikuwa maoni ya walimu
na wanafunzi kwenye hojaji. Utafiti huu utakuwa wa manufaa kwa walimu na wanafunzi
kwani ni maturnaini yangu kwamba utawaondolca utata wa.nafunzi wa shule za upili,
vyuo, vyuo vikuu na wasomaji wa riwaya za Kusadikika na Walenisi. Utata huo ni ule
unaosababishwa na matumizi ya mandhari ya kinjozi yaliyojengwa kwa misingi ya
udhahania. Utafiti huu pia ni mchango wa kial/<gg;leQ1Vi#a kwa eneo la mandhari katika
fasihi ya Kiswahili. Matgkeo ya utafiti huu yalithibitisha kwamba riwaya za Kusadikika
na Walenisi zina mandhari ya kinjozi yenye sifa bainifu. Baadhi ya sifa bainifil za mbinu
ya mandhari ya kinjozi ni: mahali pa kidhahania, ufumbaji kipindi, chuku, unyume na
matumizi ya istiara. Pia ilibainika kuwa mbinu ya rnandhari ya kinjozi imetumiwa
kisanii kumulika matatizo ya ja.mii katika riwaya hizo mbili. Matokeo pia yalionyesha
kwamba matumizi ya mbinu ya mandhari ya kinjozi yalisababisha utata katika
Kusadikika na Walenisi. Vile vile matokeo ya uchunguzi huu yalionyesha kwamba
waandishi Wa Kusadikika na Walenisi Kusadikika na Walenisi walitumia mandhari ya
kinjozi katika kazi zao ili kuepuka kazi hizo kukaguliwa kwa ukali na kudhibitiwa na
serikali zilizokuwa Zikitawala wakati huo.