Abstract:
Utafiti huu ulichunguza ukalimani katika mikutano ya kidini na hasa kama ujumbe uliowasilishwa katika lugha lengwa ni uleule uliokusudiwa katika lugha chanzi. Malengo ya utafiti huu yalikuwa kuchunguza ukalimani kutoka Kiingereza hadi Kiluo na Kiluo hadi Kiswahili ili kubainisha visababishi vya matatizo katika ujumbe kwenye kalimani. Utafiti huu ulizingatia Nadharia ya Nida ambayo mbali na kueleza maana ya tafsiri, inazungumzia umuhimu wa mazingira na utamaduni katika tafsiri na pia sifa zinazomfaa mtu anayetaka kufanya kazi ya tafsiri. Deta ilikuwa tunukuzi za mahubiri na ukalimani wake na maoni ya hadhira kwenye hojaji. Utafiti huu utakuwa wa manufaa kwa Watafiti wa kalimani hasa katika upande wa mbinu na nadharia. Ulinganishi wa lugha zinazohusika utabainisha tofauti za kimiundo za lugha husika. Pia mianya itajitokeza ya kufanyia utam‘ "W katika nyanja hii ya ukalimani.TumeWasilisha kazi hii katika sura tano. Sura ya kWaAlLG Au Jjenzi Wa Utafiti.Sura ya pili ina Mapitio ya Maandishi pamoja na Msingi wa Nadharia‘ Katika sura ya tam tumeonyesha mbinu tulizotumia kufanyia utafiti. Sura ya nne ina Matokeo ya Uchunguzi na hatimaye katika sura ya tano tumetoa Muhtasari kwa ujumla, Hitimisho na Mapendekezo.