Abstract:
Utanzu wa Fasihi Simulizi ya Kiafrika ulipuuzwa kwa namna fulani na Wataalamu wengi wa kigeni. Wengi wa Wataalamu hao hawakuona chochote chenye manufaa katika Fasihi Simulizi ya Kiafrika. Ni dhahiri kuwa kauli hiyo ilitolewa na Wataalamu hao, kama vile Finnegan (1970) na Beuchat (1965), bila ya utafiti wa kutosha kuhusu umuhimu wa Fasihi Simulizi kalika muktadha wa kijamii. Uwezekano m)wingine ni kuwa Wataalamu hao walifanya uchunguzi wao. huku tayari wakiwa wameshafikia uamuzi wao, ambao bila shaka uliathiri matokeo ya uchunguzi wao. Vile vile hatuwezi kupuuza uwezekano mwingine kuwa, Wataalamu hao walishindwa kubainisha tanzu mbali mbali za Fasihi Simulizi na Umuhimu wa tanzu hizo katikajamii. Ili kuonyesha umuhimu wa Fasihi Simulizi ya Kiafrika_ tasnifu hii imeingilia vilivyo utanzu wa visaasili. Tasnifiz hii imejikita katika kueleza maana, matumizi ya visaasili vya Wakikuyu, na kutizama sifa mbalimbali za usanaa zinazotambulisha visaasili kama utanzu maalum na wenye umuhimu mkubwa katika Fasihi Simulizi. Katika kutekeleza lengo hiIo_ nimeigawanya tasnifu hii kwenye sura tano maalum ambazo pia zina visehemu mbalimbali m niweze kushugulikia kikamilifu kila kipengele miongoni mwa hivyo nilivyotaja. Licha ya kuwa visaasili huburudisha hadhira, visaasili aidha hutekeleza jukumu muhimu zaidi la kuwafunza watoto na vijana au hata watu wazima na kuwaelimisha juu ya mambo mbalimbali yanayohusu maisha ya jamii. Visaasili hutoa mafunzo muhimu kuhusiana na matukio au maumbile ya mambo mbalimbali katikajamii. Sura ya kwanza ni utangulizi wa jumla kuhusu kile ambacho kimo katika tasnifu nzima. Katika sura hii, some la utafiti, madhumuni na jinsi ambavyo madhumuni hayo yalivyo, ni miongoni mwa mambo muhimu ambayo yamejadiliwa. Utanzu wa visaasili ni miongoni mwa tanzu nyingine za hadithi zilizomo katika Fasihi Simulizi. Ili tanzu hizo za hadilhi zieleweke vilivyo. sura ya pili imejikita katika kutoa maelezo kuhusu tanzu mbalimbali za hadithi. Aidha katika sura ya pili kuna mambo muhimu yanayohusiana na utambaji hadithi miongoni mwa Wakikuyu. Wakati na mahali mwa utambaji_ na aidha sheria zilizohusu utambaji zimetolewa maelezo. Katika sura ya tam, matumizi mbalimbali ya visaasili katika jamii ya Wakikuyu yameelezwa. Kwa mfan0_ umuhimu wa visaasili umeangaliwa kwa undani sana, huku mifano ya visaasili au vielelezo vya mafunzo vikitolewa. Kwa upande wa namna ya matumizi ya visaasili katika jamii ya Wakikuyu, kuna maelezo kwa undani ya yale manufaa yanayokusudiwa ama ujumbe unaotarajiwa kuifikia hadhira na hivyo kuinufaisha kwa njia ya kielimu na kijamii (mafunzo ya kitaaluma na kijamii) Sura ya nne imejadili sifa au mbinu za visaasili vya Wakikuyu katika kueleza usanaa unavyojitokeza katika visaasili mbalimbali vilivyochambuliwa. Sura ya tano ni hitimisho Ia tasnifu hii. Katika sura hii, muhtasari wa mambo muhimu yanayobainika katika tanifu nzima umetolewa, kisha msimamo wa tasnifu pamoja na mapendekezo mbalimbali kwa wasomi na wapangaji sera za elimu yametolewa.