Please use this identifier to cite or link to this item: http://41.89.96.81:8080/xmlui/handle/123456789/3045
Title: Kung za kiundishi za kimajaribio katika riwaya teule za kisasa za Kyallo Wadi Wamitila
Authors: Mwikali, Janice Mutua
Keywords: Riwaya Teule
Issue Date: Jun-2023
Publisher: Egerton University
Abstract: Riwaya za kimajaribio ni kazi andishi za kibunifu zilizoandikwa kwa kufuata mitindo mipya ya uandishi Wa riwaya za kisasa ambapo mbinu zinazotumiwa hukiuka uhalisia Wa kihistoria Wa kijadi hasa katika uwasilishaji wa vitushi. Kwa kuwa wasanii wana uhuru wa kuandika jinsi Wapendavyo, matumizi ya mbinu za majaribio yamepelekea kuibuka kwa riwaya mpya ya Kiswahili inayoegemca mkondo wa “uhalisia-mpya.” Wamitila ni mmojawapo wa waandishi wa riwaya za Kiswahili anayetumia mbinu za kimajaribio kama kunga ya uandishi Wa bunilizi zake za kisasa. Kiini cha utafiti huu kilikuwa kubainisha namna mwandishi anavyozitumia mbinu za kimajaribio kama msingi mkuu Wa ubunifu katika riwaya anazozibuni. Vilevile, utafiti huu uliazimia kubainisha mbinu mahususi anazotumia Wamitila kuangazia maswala yanayoibuka katika jamii. Kuafikia haya, riwaya tatu za mwandishi zimeteuliwa kimaksudi. Ni pamoja na: Musaleo, Msichamz wa Mbalamwezi na Mwandishi, Msomaji na Mchapishaji. Mtafiti ameweka bayana mbinu za kimajaribio anazotumia Wamitila kwa kuzitambulisha na kufafanua vipengele mbalimbali vya mbinu husika katika riwaya teule. Aidha, utafiti ulichunguza jinsi mbinu hizo zilivyotumika kama kunga ya uandishi na kifaa cha kuwasilishia ujumbe katika riwaya za kisasa. Utafiti uliongozwa na nadharia ya usasaleo kama ilivyoasisiwa Jean-Francois Lyotard, Jean Baudrillard, Jurgen Habermas na Fredric Jameson. Kwa mujibu Wa nadharia ya usasaleo utaratibu maalum wa kijamii uliozoeleka huyumbishwa. Nadharia hii inakiuka matumizi ya riwaya kuu ya kihalisia na kupendekeza kutumika kwa riwaya mpya iliyojawa na uradidi unaoleta maana pana kama njia ya kuelezea maswala muhimu ya jamii. Kwa kuwa data iliyokusanywa ilikuwa ya kithamano, mtafiti alisoma riwaya teule za mwandishi na kudondoa mbinu mbalimbali za kimajaribio zilizotumika katika bunilizi husika. Utafiti ulibaini kuwa Wamitila amewasilisha maswala mahususi yanayohusu jamii kwa kutumia mbinu za kimajaribio kama kunga yake ya ubunifu. Hatimaye, mtafiti alibaini kuwa simulizi fupi, urcjeleomatini, taashira, dayolojia, uhalisiajabu, tamathali za lugha ndivyo vipengele vikuu vya kimajaribio vinavyokatiza usimulizi katika riwaya teule. Utafiti huu umesisitiza kuhusu jinsi waandishi wa riwaya ya kisasa ya Kiswahili Wanavyoyasawiri maswala ya kijamii katika bunilizi zao. Matokeo ya utafiti ni nyongeza kwa taaluma ya ujuzi na ufahamu unaohusu kunga za uandishi wa kazi za fasihi. Aidha, ni mchango katika kuwaelekeza Waandishi na Wasomaji kuhusu uelewa Wa mbinu za kimajaribio kama kunga ya kuwasilisha dhamira na maudhui katika riwaya ya Kiswahili
URI: http://41.89.96.81:8080/xmlui/handle/123456789/3045
Appears in Collections:Faculty of Education and Community Studies

Files in This Item:
File Description SizeFormat 
Kung za kiundishi za kimajaribio katika riwaya teule za kisasa za Kyallo Wadi Wamitila.pdfThesis2.31 MBAdobe PDFThumbnail
View/Open


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.