Please use this identifier to cite or link to this item: http://41.89.96.81:8080/xmlui/handle/123456789/3208
Title: Lugha na mitazamo ya wazungumzaji wa kĩndia na kĩgĩchũgũ kuhusu utambulisho wao wa kijamii
Authors: Ndung'u, Peris, Mwihaki
Keywords: Kiwsahili
Issue Date: Mar-2023
Publisher: Egerton University
Abstract: Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa uhai, fikra na nguvu ya kuandika na kuikamilisha tasnifu hii. Pili, ninatoa shukrani za pekee kwa wasimamizi wangu katika utafiti huu Dkt. Raphael Gacheiya na Prof. Catherine Kitetu kwa kukubali kuchukua jukumu la kusimamia kazi hii. Ninawashukuru kwa uvumilivu wao tokea hatua ya kuandaa pendekezo la utafiti hadi kukamilika kwa tasnifu. Nawashukuru kwa mafanikio na juhudi yao ya kusoma, kukosoa na kunishauri kwa umakini hadi kuhitimisha. Hata ingawa walikuwa na majukumu mengine, hawakusita kusoma kazi yangu na kunielekeza kwa subira. Ninawaombea dua kwa Mwenyezi Mungu awazidishie katika maisha yao ili waweze kuendelea kuwafaidi wengine katika masomo yao. Pia namshukuru msimamizi wangu wa hapo awali, Prof. Furaha Chai kwa mchango wake ulionifaa katika pendekezo la utafiti. Namuombea kheri katika Chuo Kikuu cha Pwani. Tatu, ningependa kushukuru uongozi wa chuo Kikuu cha Egerton kwa kunipa fursa ya kuzamia katika masomo yangu. Ninawashukuru wahadhiri wote katika idara ya Fasihi, Lugha na Isimu kwa mchango, wosia na mawaidha yao wakiwemo mwenyekiti wa idara Dkt. Walunywa, mwenyekiti wa awali katika idara Dkt. Kweya, pamoja na wahadhiri Prof. Bartoo, Dkt.Taib, Bw. Muindi, Bw. Kahiro, Bw. Kwambai na wengineo. Mungu awazidishie ili waendelee kuwafaa wengine kielimu na kitaaluma. Nne, ninatoa shukurani za dhati kwa wanafunzi wenzangu, Melvin Ouma, Mildred Abonyo, Geoffrey Kibet na Victor Gatimu kwa ushirikiano wao katika masuala ya kitaaluma kwa kipindi chote cha masomo. Nawaombea fanaka kiakademia na katika maisha yao. Tano, ninatoa shukrani za dhati kwa mama yangu Bi. Margaret Wambui kwa malezi na mapenzi yake, maombi na kuwa na imani kwangu. Shukrani kwa baba na mama mkwe, Bw. na Bi. Kanyingi kwa kunipa motisha kila wakati na kunihimiza kujitahidi nisife moyo. Naishukuru wake. Shukrani kwa watoto wetu, Elvis Kanyingi, Lucius Ndung’u na Amirah Mugure kwa mapenzi na uvumilivu wao wakati wote wa masomo yangu. Vile vile, shukrani zangu ziendee familia ya mjomba, Bw. na Bi. Mbogo Robert kwa kufadhili masomo yangu ya shahada ya kwanza, Mungu awabariki na awalinde siku zote. Mwisho, nawashukuru Purity Muthoni na Bw. Kabiru waliokuwa watafiti wasaidizi wangu. Walikuwa wa msaada kwangu katika ukusanyaji na uchanganuzi wa data. Kwa wengine ambao kwa njia moja au nyingine walinisaidia katika kufanikisha kazi hii, nawashukuru nyote Mungu awabariki. ASANTENI SANA.
URI: http://41.89.96.81:8080/xmlui/handle/123456789/3208
Appears in Collections:Faculty of Education and Community Studies

Files in This Item:
File Description SizeFormat 
Lugha na mitazamo ya wazungumzaji wa kĩndia na kĩgĩchũgũ.pdfThesis2.48 MBAdobe PDFThumbnail
View/Open


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.