Please use this identifier to cite or link to this item: http://41.89.96.81:8080/xmlui/handle/123456789/3937
Title: Usawiri wa Wahusika Watoto katika Tamthilia Zilizopendekezwa katika Shule ya Ulili,Visiki na Amezidi
Authors: Bowen, Dave .K.
Keywords: Visiki na Amezidi
Tamthilia
Issue Date: 2003
Publisher: Egerton University
Abstract: Utafiti huu umeshughulikia usawiri wa Wahusika watoto katika tamthilia za na Amezidi. Lengo kuu la utafiti huu ni kuangalia namna Wahusika watoto walivyochorwa na kuchunguza mtamzamo wa watu wazima kuhusu watoto katika tamthilia husika. Ripoti hii imegawanywa katika sura tano. Sura ya kwanza, inazingatia ufafanuzi wa mada ya utafiti, madhumuni ya utafiti, nadharia tete, sababu ya kuchagua mada, umuhimu wa utafiti na upeo wa utafiti. Sura hii pia imetoa maelezo juu ya nadharia inayotumika pamoja na yaliyoandikwa kuhusu mada. Mbinu zinazotumika katika utafiti huu pia Zinaelezwa katika sura hii. Sura ya pili, inatoa kwa muhtasari maisha ya waandishi S.A Mohamed na Khaemba Ongeti. Vilevile inagusia ufafanuzi wa dhana ya wahusika na uwasilishaji wa Wahusika na aina mbalimbali za wahusika. Haya yote ni muhimu katika kuangalia namna Wahusika watoto walivyosawiri katika Visiki na Amezidi. Sura ya tatu, inajihusisha na mtamzamo wa Ngara (1982) kuhusu wahusika katika kazi ya sanaa. Aidha tunaangazia Wahusika na Iugha, na mwandishj na Wahusika wake. Sura ya nne, ndicho kitovu cha utafifi wem. Hapa ndipo utafiti unaangazia vile Wahusika watoto wamesawiri katika mazingira mbalimbali. Kwa ujumla, waandishi wamesawiri wahusika wakiwa na sum mbalimbali. Haya yote ni kwa sababu waandishi wote walitoka katika mazingira tofauti. Hata hivyo walizingatia uhalisia Wa rnaisha yaliyowazingira. Hatimaye, sura ya tano, inahusu muhtasan' wa ripoti nzima, matokeo na hifimisho la utafiti. Aidha sura hii inaangazia matatizo yaliyokumba utafiti pamoja na kutoa mapendekezo juu ya tafiti zaidi za baadaye, kuhusu Wahusika watoto katika kazi za fasihi.
URI: http://41.89.96.81:8080/xmlui/handle/123456789/3937
Appears in Collections:Faculty of Arts and Social SciencesItems in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.