Please use this identifier to cite or link to this item: http://41.89.96.81:8080/xmlui/handle/123456789/3974
Title: Hali ya Kiswahili Katika Elimu Nchini Rwanda
Authors: Kimenyi, Thaddee, R
Keywords: Kiswahili -- Elimu -- Rwanda
Issue Date: Jan-2003
Publisher: Egerton University
Abstract: Utangulizi - Utafiti huu ulijishughulisha na kuchunguza hali ya lugha ya Kiswahili katika elimu nchini Rwanda. Utafiti ulishughulikia zaidi vipingamizi vinavyokwamiza uendelezaji wa lugha ya Kiswahili katika elimu nchini Rwanda. Hii haina maana lovamba wananchi wa Rwanda hawazungumzi wala kupenda lugha hii. La hasha. Kinyume chakc, lugha hii iliingizwa nchini Rwanda zaidi ya miaka mia moja iliyopita. Hakika kabisa “Kiswahili kiliingia nchini Rwanda kwa mara ya kwanza mwishoni mwa kame ya 19 kati ya tarehe ll na tarehe 15 Disemba 1892” (Ntawigira.1997). Matumizi ya Kiswahili nchini Rwanda siyo makubwa ukilinganisha na nchi jirani za Afrika Mashariki na hata zile za Afrika ya Kati kama vile Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kiswahili kinachozungumzwa nchini Rwanda kwa wingi ni Kingwana, lahaja ya Kiswahili inayotumiwa RDC husasan masahriki mwa nchi ya Congo (Chimerah, 2000). Swali muhimu Ia utafiti huu ilikuwa ni kuona ni kwa nini Kiswahili katika elimu nchini Rwanda hakitumiwi vilivyo ilhali ndiyo lugha ngeni ya kwanza kufika Ru anda kwa muda \va zaidi ya miaka mia moja iliyopita (Karangira 198611 18).
URI: http://41.89.96.81:8080/xmlui/handle/123456789/3974
Appears in Collections:Faculty of Arts and Social Sciences

Files in This Item:
File Description SizeFormat 
Hali ya Kiswahili Katika Elimu Nchini Rwanda.pdf15.59 MBAdobe PDFThumbnail
View/Open


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.