Please use this identifier to cite or link to this item: http://41.89.96.81:8080/xmlui/handle/123456789/3976
Title: Uchanganuzi wa Matumizi ya Lugha Katika Magazeti ya Kiswahili Nchini Kenya: Mfano wa Gazetti la Taifa Leo
Authors: Ontieri, James, Omari
Keywords: Matumizi ya Lugha -- Magazeti ya Kiswahili -- Taifa Leo
Issue Date: Jun-2005
Publisher: Egerton University
Abstract: Magazeti ni chombo muhimu katika usambazaji wa habari kote ulimwenguni. Gazeti la Tazfiz Leo linalochapishwa nchini Kenya lina umuhimu wa kipekee kama chombo mahsusi cha kuwasilishia ujumbe kwa Wakenya wengi kwani huandikwa kwa Kiswahili ambayo ni lugha ya taifa; yenye matumizi mapana na inaeleweka miongoni mwa wananchi wengi. Hata hivyo, utafiti umeonyesha kuwa mammizi ya lugha yenye upungufu wa ufasaha katika uandishi wa makala yachapishwayo katika gazeti hili, ni jambo mojawapo linalopelekea gazeti hilo kumsomwa na walu wengi. Utafiti huu umechunguza rnatumizi ya lugha katika Tazfiz Leo huku makosa mahsusi yanayojitokeza katika makala mule yakitambulishwa na kujadiliwa Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Uhakiki wa Kimtindo. Katika utafiti huu, nakala thelathini za gazeti la Taifiz Leo zilizochapishwa kati ya 1999 na 2003 zilichanganuliwa ili kugundua jinsi ambavyo lugha imetumiwa kuwasilishia ujumbe kwa hadhira Mtindo wa sampuli shelabela na ile iliyoazimiwa ulitumiwa katika kuteua nakala zilizochanganuliwa. Njia ya utafiti ya upekuzi wa kimaktaba ilitumiwa ambapo mbinu ya uchanganuzi umbo-maana ilizingatiwa katika kukusanya data Data iliyokusanywa ilipangwa kulingana na nadharia tete za utafiti na kuchanganuliwa kwa kuzingatia umara-wkezi wa makosa katika vipengele vya lugha vilivyochunguzwa Uchanganuzi umeonyesha kuwa kuna makosa mengi katika vipengele mahsusi vya lugha vilivyochunguzwa mathalan: Samfi, Msamiati, Methali, Nahau na Tamathali za Usemi. Tunammai kuwa matokeo ya utafifi huu, yatawafaa waandishi na wachapishaji wa magazeti, hususan Taifiz Leo, katika juhudi za kuchunguza mbinu zao m uandishi kwa mujibu wa makosa yaliyotambulishwa ili kuimarisha mawasiliano. Matokeo haya huenda pia yakachangia katika kuweka misingi ya utarnbulishaji na uchanganuzi wa makosa katika Kiswahili na hivyo kuwanufaisha walimu na wanafunzi katjka viwango rnbalimbali vya mafunzo katika harakati mo za kuepukana na makosa yatokeayo katika uandishi. Aidha, ustawishaji na uenezaji wa Kiswahili kama lugha ya taifa nchini Kenya, utasukumwa mbele.
URI: http://41.89.96.81:8080/xmlui/handle/123456789/3976
Appears in Collections:Faculty of Arts and Social SciencesItems in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.