Please use this identifier to cite or link to this item: http://41.89.96.81:8080/xmlui/handle/123456789/3977
Title: Tofauti za Umenke Katika Mazungumzo ya Darasani: Utafiti katika Shule Mbili za Upili, za Mseto Wilaya ya Kilifi - Kenya
Authors: Noah, Wafula, Christopher
Keywords: Umenke -- Mazungumzo ya Darasani
Issue Date: Jan-2002
Publisher: Egerton University
Abstract: Utafiti huu, umeshughulikia mazungumzo ya darasani kati ya mwalimu na wanafmqzi ili kudhihirisha iwapo kuna usawa wa umenke kati ya wavulana na wasichana wanaoshiriki. Ingawa wanafunzi damsani huwa sawa, wanaisimu waliochunguza umenke darasani wanasema kuwa wasichana na wavulana wamekuwa wakihudmniwa tofauti katika mazungumzo ya darasani. Jambo hili, kulingana na utafiti katika nchi za ulaya, limechangia kutokuwepo kwa usawa, na mara nyingi wasichana huhasirika kwa kutopata nafilsi ya kushiriki kikamilifi1 katika mazungumzo. Wasomi wanakubaliana kuwa mazungumzo ni kifha muhimu sana katika upataji elimu. Kupitia mazungumzo, tunapitisha mawazo yetu kwa wengine, tunatalii mawazo mbalimbali, tunayathibitisha, na kuyafanya kuwa yetu: Utafiti huu ulichunguza na kubainisha ni nani wanaotawala mazungumzo ya darasani, na majukumu ya wahusika mbalimbali katika kuendeleza utawalaji wa mazungumzo hayo. Pia, utafiti huu, ulichunguza utaratibu wa kutoa nafiisi za kuzungumza kwa wanafunzi na jinsi unavyoendeleza utawalaji wa mazungumzo. Utafiti huu ulijibana katika muktadha wa shule mbili za upili za mseto ambapo masomo ya Kiswahili na Kiingereza yalichunguzwa. Mtafiti alitumia misingi ya nadharia za Kiisimu za Uelemea Kike katika mtazamo wa Mwelekeo Lemevu. Matokeo ya utafiti huu yametuwezesha kufahamu vyema wanaotawala mazungumzo ya darasani, na sababu za hali hiyo. Ni matumaini yetu kuwa, utafiti huu utawafaidi walimu, mashifika mbalimbali yanayopigania usawa wa wanawake na wanaume, pamwe na wapangaji sera za eiimu, hasa katika mijadala inayohusu ubora wa shule za mseto na zile zisizo za mseto.
URI: http://41.89.96.81:8080/xmlui/handle/123456789/3977
Appears in Collections:Faculty of Arts and Social Sciences



Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.