Please use this identifier to cite or link to this item: http://41.89.96.81:8080/xmlui/handle/123456789/3978
Title: Uchanganuzi wa Namna Burhani Anavyotatua Matatizo Yanayokabili Jamii Katika Riwaya Zake
Authors: Rotich, Peter, Kibet
Keywords: Uchanganuzi -- Burhani -- Matatizo -- Jamii -- Riwaya
Issue Date: Jun-2005
Publisher: Egerton University
Abstract: Jumuiya ya binadamu daima haikosi kuwa na matatizo ambayo huambatana na migongano ya aina mbalimbali. Ili kuishi maisha yenye amani na salarna binadamu hutafuta mikakati ya kutatua matatizo yake. Waandishi wa riwaya, Burhani akiwa mmoja wao, husawiri hali hii katika kazi zao. Riwaya za Burhani hazijashughulikiwa sana na utafiti huu ulilenga kubainisha namna anavyosawiri hali hiyo. Utafiti ulichanganua riwaya za Burhani; Mali ya Maskini (1981) na Mwisha wa Kosa (1987). Ulichanganua namna ambavyo Burhani anatatua matatizo ya jamii anayoyamulika katika riwaya zake. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kuthibitisha mambo mawili. Kwanza ni kwamba, Burhani amernulika matatizo mbalimbali katika riwaya zake, yaani hakujifunga katika matatizo ya namna moja. Pili, ilikuwa ni kubainisha mikakati mbalimbali aliyotumia katika utatuzi wa rnatatizo hayo. Kwa sababu matatizo yote yaliyomulikwa yamejengeka katika migongano ya namna mbalimbali, utafiti huu ulizingatia nadharia ya mgongano ambayo iliasisiwa na Karl Man; na mikakati iliyopendckezwa na wanasosiolojia ya kuondoa migongano inayozushwa na matatizo hayo. Katika utafiti huu nilitumia utaratibu wa upckuzi wa yaliyomo katika ukusanyaji wa deta. Katika uchanganuzi Wa deta, utafiti uliturnia mbinu ya kithamano ambapo nilichanganua deta ya matukio yanayodhihirisha rnatatizo na namna ambavyo mwandishi anatumia mikakati mbalimbali katika juhudi za kuondoa matatizo hayo. Matokeo ya utafiti huu yaliweza kuthibitisha kuwa, Burhani amemulika matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii, kama vile; umaskini, mkengeuko, ufisadi, kudhibitiwa kwa mwanamke katika ndoa na chuki. Pili, amependekeza mikakati mbalimbali katika utatuzi wa matatizo hayo, kama vile; kutambua tatizo, kulizungumzia tatizo, kushauriana na kupatana. Mikakati hiyo ilipokosa kufaulu, asasi za jela na mahakama zilitumika. Utafiti huu ulifichua mengi kuhusu matatizo anayoyamulika Burhani katika jarnii. Aidha utafiti huu utawachochea watafiti wa siku za usoni wafichue zaidi kuhusu Burhani kama mwandishi na riwaya zake.
URI: http://41.89.96.81:8080/xmlui/handle/123456789/3978
Appears in Collections:Faculty of Arts and Social Sciences

Files in This Item:
File Description SizeFormat 
Uchanganuzi wa Namna Burhani Anavyotatua Matatizo Yanayokabili Jamii Katika Riwaya Zake.pdf28.37 MBAdobe PDFThumbnail
View/Open


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.