Please use this identifier to cite or link to this item:
http://41.89.96.81:8080/xmlui/handle/123456789/3979
Title: | Mifanyiko ya Kifonolojia Katika Kinyala cha Kakamega |
Authors: | Ngero, Siteti |
Keywords: | Mifanyiko ya Kifonolojia |
Issue Date: | 1996 |
Publisher: | Egerton University |
Abstract: | Tasnifu hii imejadili mifanyiko ya kifonolojia katika Kinyala cha Kakamega, hususan jinsi mifanyiko hiyo inavyodhihirika kwa kuiundia kanuni zinazoitawala. Kazi hii, mbali na kuziainisha sauti za Kinyala (K), inaibua fiuundo wa kifonolojia wa lahaja hii. Ni kutokana na uainishaji wa sauti na uibuaji wa muundo wa kifonolojia ndipo yeyote yule atakaye kujifunza an kufunza lahaja hii anaweza kufanya hivyo kwa utaratibu ufaao. Mifanyiko ya kifonolojia katika Kinyala cha Kakamega ndio lengo la tasnifu hii. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti huu. Miongoni mwa mambo mengine, some la utafiti limejadiliwa, madhumuni ya utafiti na pia sababu za kglichagua some hili. Zaidi ya hayo, nadharia ambayo imetumiwa kama msingi wa utafiti huu imezungumziwa. Mwisho, njia za utafiti ambazo zilitumiwa kufanikisha utafiti huu zimejadiliwa. Sura ya pili inajadili maandishi mbalimbali yanayohusiana na some hili. Sura ya tatu. inajadili sauti za Kinyala cha Kakamega. Hii inatokana na dhana inayosisitizwa na Mario Pei (l965:ll) kwamba ambapo fonolojia inaweza kufafanuliwa kama uchunguzi wa sauti za lugha vile zinavyobadilika na kugeuza umbo katika maendeleo ya lugha, fonetiki ndiyo sayansi, uchunguzi, uchanganuzi na utabakishaji wa sauti za lugha bila kurejelea maendeleo yake kihistoria; lakini kwa kurejelea utamkaji, uenezaji na upokeaji wake. Yaani, fonolojia na fonetiki huchanganiana kiasi kwamba ni vigumu kuzungumzia fonolojia bila kurejelea fonetiki. Hivyo basi, katika sura hii, mfumo wa kifonetiki wa Kinyala cha Kakamega umejadiliwa na kuziainisha sauti zote za lahaja hii — konsonanti na vokali. Sura ya nne imejadili mifanyiko ya kifonolojia katika Kinyala cha Kakamega. Sura hii imejaribu kuonyesha jinsi na pale ambapo mifanyiko hiyo hutokea na kuieleza kiisimu. Katika kufanya hivyo, iliundiwa kanuni mwafaka zinazoambatana nayo (mifanyiko). Sura ya tano ni ya kuhitimisha. Sura hii imepitia kazi yote kwa jumla na kuonyesha kwamba Kinyala cha Kakamega hudhihirisha mifanyiko ya kifonolojia ya aina nane. Fauka ya hayo, matatizo yaliyoukumba utafiti huu yamejadiliwa na kutoa mapendekezo ya maswala ambayo yanastahili kufanyiwa utafiti zaidi. |
URI: | http://41.89.96.81:8080/xmlui/handle/123456789/3979 |
Appears in Collections: | Faculty of Arts and Social Sciences |
Files in This Item:
File | Description | Size | Format | |
---|---|---|---|---|
Mifanyiko ya Kifonolojia Katika Kinyala cha Kakamega.pdf | 34.33 MB | Adobe PDF | ![]() View/Open |
Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.