Please use this identifier to cite or link to this item: http://41.89.96.81:8080/xmlui/handle/123456789/3424
Title: Fani katika hadithi fupi za kiswahili
Authors: Mohochi, Sangai E.
Keywords: Fani katika hadithi fupi za kiswahili
Issue Date: 1995
Publisher: Egerton University
Abstract: Tasnifu hii imejishughulisha na uhakiki wa fani katika hadithi fupi za Kiswahili ikiwa na lengo la kudhih;risha kuwa aiwa hii ya sanaa ni utanzu mahsusi wa fasihi wenye kaida mbalimbali zinazoongoza ijenzi wa fani yake na kuutofautisha na kazi nyingine. Utafiti huu ulichochcwa na utambuzi kuwa hadithi fupi haijafanyiwa uhakiki kama kazi nyingine za fasihi. Aidha, katika fasihi ya Kiswahili kwa jumla, fani haijatafitiwa kama maudhui. Swala la kimsingi katika tasnifu hii ni uchunguzi wa fani katika hadithi fupi. Japo hivyo, tumegusia kimuhtasari tu maudhui muhimu yanayowasilishwa na wasanii wa hadithl zilizohakikiwa kwani, kimsingi, fani na maudhui ni vipengele ambavyo hukamilishana. Ili kuyafanikisha.malengo ya tasnifu hii, tumeteua hadithi nne kuwa msingi wa uhakiki huu. Hadithi zenyewe ni: "siri ya Bwanyenye", "Wasubiri Kifo", "Kicheko cha Ushindi" na "Msiba wa Pamoja". Tasnifu hii imegawanywa katika sura sita. Sura ya kwanza ni utangulizi na imeeleza mada ya tasnifu, madhumwni ya utafiti, umuhimu wa mada hii, nadharia iliyotawala uchunguzi huu, upeo wake pamoja na yaliyoandikwa kuihusu mada hii. Sura ya pili ni muhtasari wa usuli na maendeleo ya hadithi fupi tangu enzi ya masimulizi hadi sasa. Tumechunguza pia athari ya ngano katika hadithi fupi andishi kifani na kimaudhui na, mwishoni mwa sura hii, tumejadili athari za jamii ya mwandishi katika utunzi wake wa kazi za sanaa. Sura ya tatu imejikita katika dhana ya hadithi fupi. Hapa tfimechunguza baadhi ya sababu zilizochangia kubaki nyuma kwa hadithi fupi na kujaribu kulijadili swala tata la maana ya hadithi fupi. Aidha, tumeyahakiki maoni ya watafiti mbalimbali kuhusu hadithi fupi, dhima na umaarufu wake karika jamii, kabla ya kuhitimisha na baadhi ya mageuzi ama mabadiliko yanayoikumba hadithi fupi andishi. Kiini cha tasnifu hii kinajitokeza wazi zaidi katika sura ya nne na ya tano kwani katika sura hizo tunahakiki vipengele mbalimbali vya fani vilivyoteuliwa kwa minajili ya utafiti huu. Sura ya nne inamulika kipengele cha lugha na, zaidi ya maelezo ya kijumla kuhuéu lugha na fasihi, sura hii imehakiki matumizi ya kunga mbalimbali za lugha katika hadithi fupi za Kiswahili. Katika sura ya tano wahusika wamechunguzwa kwa undani, kwanza katika fasihi kwa ujumla na, hatimaye, katika haditbi fupi. Tumeonyesha kuwa uumbaji na uwasilishaji wa wahusika katika haaithi fupi unatoa mchango usio haba katika kuitambulisha na kuitofautisha hadithi fupi. Wasanii wengi wanawaeleza wahusika wao na, kutokana na ufinyu wa mawanda, wahusika wengi hawakuzwi hatua kwa hatua na kuimarika vilivyo. Sura hii pia inachunguza ploti na usimulizi kama vipengele muhimu vya fani ya hadithi fupi. Hadithi fupi imedhihirisha kuwa na ploti sahili ambayo, aghalabu, huwa na msuko wa moja kwa moja na rahisi kufuatilia. Pili, inatumia mbinu mbalimbali za usimulizi lakini ile ya usimulizi maizi imejitokeza zaidi. Katika sura ya sita ambayo ni hitimisho, tumetoa muhtasari wa kiini cha tasnifu nzima kwa kugusia, kimuhtasari, maswala yaliyoshughulikiwa kisha tukatoa hitimisho pamoja na mapendekezo yetu. Tumeeleza pia kwamba kuna vipengele kadhaa muhimu vya fani ambavyo hatukuweza kuvihakiki katika upeo wa tasnifu hii.
URI: http://41.89.96.81:8080/xmlui/handle/123456789/3424
Appears in Collections:Faculty of Arts and Social Sciences

Files in This Item:
File Description SizeFormat 
Fani katika hadithi fupi za kiswahili.pdf2.13 MBAdobe PDFThumbnail
View/Open


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.